TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 12-02-2020

Manchester United iko tayari kuipiku Chelsea katika kinyang'anyiro cha kutoa dau la £120m kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Mirror)
Liverpool inajiandaa kumpatia beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, 28, mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya £150,000 kwa wiki. (Football Insider)

Manchester United inaweza kufufua hamu yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 Moussa Dembele mwisho wa msimu huu (L'Equipe, via Manchester Evening News)
Tottenham inaandaa dau la £40m ili kujaribu kumsajili beki wa kati wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, (Express)
Mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, ana uwezekano mkubwa kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu huku Chelsea, Manchester United na Arsenal zote zikipigania saini yake. (Mail)
Chelsea Itamchunguza mchezaji wa Morocco Hakim Ziyech kwa kipindi cha msimu kilichosalia ili kuweza kumnunua mchezaji huyo wa Ajax katika dirisha la mwezi Januari mwaka ujao.

hakim Ziyeck wa Ajax

Post a Comment

0 Comments