BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 05-02-2020

Manchester United wanajiandaa kutoa dau nono ili kumsajili kiungo wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, mwishoni mwa msimu. (Mirror)
United wanamtaka Grealish kutokana na uwezekano mkubwa kwa chaguo lao la awali James Maddison, 23, kukaribia kusaini mkataba mpya na Leicester City. (Mirror)
Klabu ya Chelsea inajipanga kumpa kocha Frank Lampard kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 23. (Evening Standard)
Paul Pogba,26, amewaambia wachezaji wenzake wa Man United kuwa bado anataka kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)
PogbaHaki miliki ya picha
Juventus wanatathmini juu ya kumsajili winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, ambaye pia anawindwa na Bayern Munich. (Calcio Mercato, via Inside Futbol)
Kocha wa Man City Pep Guardiola anataka kusajili walinzi wa kati wawili hatua ambayo inazidi kuweka wingu jeusi kwa mustakabali wa beki wa England John Stones, 25. (Times, subscription required)
Wakala wa winga Gareth Bale, 30, amekanusha kuwa Tottenham ilituma ofa ya usajili kwa klabu ya Real Madrid kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Talksport)
Manchester United wanatarajia kipa wao raia wa Argentina Sergio Romero, 32, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu sambamba na kipa wao namba tatu Lee Grant, 37. (Sun)
Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Feyenoord na Uturuki Orkun Kokcu, 19. (Mail)
Moussa DembeleHaki miliki ya picha
Kocha Manuel Pellegrini amedai kuwa kiwango kibovu cha kipa Roberto kimechangia yeye kutimuliwa kazi na klabu ya West Ham. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Leicester City na Algeria Islam Slimani, 31, "valikuwa karibu" ajiunge na klabu ya Inter Milan kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari. (Calcio Mercato, via Leicester Mercury)

Post a Comment

0 Comments