BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 27-02-2020

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ana matumaini ya kuipiku Manchester United kumsajili kiungo wa RB Leipzig Emil Forsberg, 28. (Express)Timu ya Serie A, Inter Milan imewasiliana na Tottenham kuhusu mchezaji wa nafasi ya ulinzi Jan Vertonghen, 32,

Real Madrid wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, 27 kwa kitita cha pauni milioni 126 baada ya kuachana na mshambuliaji Gareth Bale, 30 (El Desmarque, via Express)
Manchester United wanajiandaa kumuuza kiungo Jesse Lingard, 27, na Andreas Pereira, 24, kwa ajili ya kugharamia uhamisho wa kiungo Jack Grealish,24. (Express)

Arsenal imejaribu kuanzisha tena mazungumzo na Pierre-Emerick Aubameyang, mkataba wake wa sasa wa mshahara wa pauni 2000,000 unatarajiwa kwisha mwishoni mwa msimu ujao.(Times, subscription required)
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamekuwa katika mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino,28. (Echo)
Katika hatua nyingine, Liverpool wako kwenye mazungumzo na RB Leipzig na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 23. (Express)
Kocha wa Inter Antonio Conte anataka kumnyakua mmoja wa mabeki wa kushoto wa Chelsea, kati ya Marcos Alonso, 29 na Emerson Palmieri, msimu huu. (Tuttosport, via Mail)
Mshambuliaji wa Chelsea Willian, 31, anasema mkataba wa sasa wa klabu hiyo haujakidhi matakwa yake hali itaja kuwa ''ngumu''. (Esporte Interativo, via Football 365)
Roma inataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling, 30, na kiungo Henrikh Mkhitaryan, 31, kwa mikataba ya kudumu. wawili hao wanacheza kwa mkopo wakitokea Manchester United na Arsenal. (Sky Sports)

SalahHaki miliki ya picha

Arsenal, Newcastle na Southampton wanamtazama kwa karibu Hoffenheim na kiungo wa kati Florian Grillitsch, 24. (Sport Bild, via Chronicle)
Mchezaji wa nafasi ya kiungo wa Barcelona Sergio Busquets, 31, amekosoa sera ya uhamisho ya klabu hiyo ambayo imewaacha mabingwa wa ligi ya uhispania na ukame wa vipaji vipya. (ESPN)
Real Madrid inaandaa ofa ya euro milioni 70 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Napoli Fabian Ruiz 23. (Calciomercato - in Italian)
Kiungo wa timu ya taifa ya Luxembourg, Danel Sinani, 22, anayeichezea Dudelange, yuko kwenye mazungumzo na Norwich City kuhusu uhamisho msimu huu.(Eastern Daily Press)
Everton wanamlenga mchezaji wa nafasi ya ulinzi Gabriel Magalhaes, 22. (Mirror)

AubameyangHaki miliki ya picha

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Newcastle United Jamaal Lascelles, 26, amesema yuko tayari kubaki na klabu hiyo wakati wote wa kazi yake. (Chronicle)
Aston Villa na Celtic zingependa kupata saini ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa kati Jack Tucker kutoka Gillingham. (Birmingham Mail)

Post a Comment

0 Comments