BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA :WALETENI HAO MAPOLISI TUWAFUNDISHE KUCHEZA SAMBA

Klabu ya Simba chini ya Kocha Sven imeonekana tishio kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi zake huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote wa ligi tangu kocha huyo aanze kuinoa . Leo Jion Sven ataendeleza ubabe wake dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi 


Kiungo  mkabaji Mbrasil Fraga ameonekana tishio kwa timu pinzai kuokana na uwezo wake wa kukaba na hata kufunga. Kwenye mchezo dhidi ya Coastal alifunga mabao mawili na kuwa nyota wa mchezo huku Traone Santos akidhihirisha ubora wake eneo la ulinzi na kuifanya ngome ya Simba kupata clean sheet yake ya kwanza kwa michezo 7 waliyocheza hivi karibuni ambayo Pascal Wawa na Erasto Nyoni walicheza kama walinzi wa kati na kuruhusu kufungwa mabao 7 kwenye mechi 6. 

Kikosi kinachoweza kupangwa na mwalimu Sven dhidi ya Polisi Tanzania ni Aishi Manula,Shomari Kapombe ,Mohammed Hussein,Traone na Erasto nyoni kwa eneo la ulinzi. Fraga,Chama,Dilunga na Mkude wanauwezeno wa kuanza kama viungo huku Kagere na Kahata wakianza kama washambuliaji .

 Pichani ni wachezaji wa Simba wakijiandaa na mchezo huo kwenye viwanja vyao vya mazoezi Bunju


Post a Comment

0 Comments