BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI:NIYONZIMA AENDELEA KUJIMWAMBAFAI NDANI YA YANGA

YANGA SC imeungana na mahasimu wao, Simba SC kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Gwambina FC jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 


Shujaa wa Yanga SC ni kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 na ushe kwa shuti la umbali wa mita 35.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani, aliyesaidiwa na Rashid Zonga wa Iringa na Abdulaziz Ally wa Arusha, pamoja na kufungwa, Gwambina ya Daraja la Kwanza ilionyesha mchezo mzuri.


Mechi nyingine za leo za Hatua ya 16 Bora ASFC, mabingwa watetezi Azam FC nao wamekwenda robo fainali kwa ushindi mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya wenyeji, Ihefu ya Daraja la Kwanza pia kufuata sare ya 0-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Kagera Sugar pia imeshinda kwa penalti 2-0 dhidi ya KMC kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Alliance FC nayo imeitoa JKT Tanzania kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Jamhuri mjin Dodoma.
Azam FC, Yanga, Kagera Sugar na Alliance FC zinaungana na Simba SC, Ndanda FC, Namungo FC na Sahare All Stars ya Daraja la Kwanza kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Lamine Moro, Kelvn Yondan/Ally Mtoni ‘Sonso’ dk67, Said Juma ‘Makapu’, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Tariq Seif/Yikpe Gislain dk87, Mapinduzi Balama/ Mohamed Issa ‘Banka’ dk77 na Bernard Morrison.

Gwambina FC; Ibrahim Isihaka, Hamad Nassor, David Bryson, Salum Kipaga, Revocatus Richard, Anthony Matogolo, Pastory Athanas/Jimson Mwanuke dk66, Yussuf Lwenge, Meshack Mwamita/Kapama Abdallah dk60, Jacob Massawe na Rajab Athumani.

Post a Comment

0 Comments