BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI : SIMBA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU BARA

Simba SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 


Sixtus Sabilo alianza kuifungia Polisi Tanzania kipindi cha kwanza kabla ya Simba SC kuzinduka kipindi cha pili kwa mabao ya Nahodha wake, mshambuliaji John Raphael Bocco na kiungo Ibrahim Ajibu.


Kwa ushindi huo, Simba SC iliyo chini ya kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandonbroeck anayesaidiwa na mzalendo, Suleiman Matola inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 19, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya Azam FC wanaofuatia nafasi ya pili, ingawa wana mechi moja mkononi.


Sixtus Sabilo alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 23 akimchambua kipa Beno Kakolanya baada ya ya kupasua katikati ya mabeki wa Simba SC kufuatia pasi nzuri ya kiungo Hassan Maulid.

Nahodha John Raphael Bocco akisawazishia Simba SC akiwa amezidi dakika ya 57 kufuatia pasi ya kiung Mzambia, Clatous Chama – lakini refa Hance Mabena kutoka Tanga hakuwa na pingamizi.  


Mtokea benchi, kiungo Ibrahim Ajibu akaifungia Simba SC bao la ushindi dakika za nyongeza akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Kenya, Fransic Kahata.


Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Haruna Shamte, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Tairone Santos, Gerson Fraga ‘Viera’, Hassan Dilunga/ Meddie Kagere dk75, Sharaf Eldin Shiboub/Ibrahim Ajibu dk46, John Bocco, Clatous Chama na Francis Kahata.


Polisi Tanzania; Mohamed Yussuf, William Lucian ‘Gallas’, Yassin Mustapha, Mohamed Kassim, Iddi Mobby, Pato Ngonyani, Sixtus Sabilo, Hassan Maulid/Andrew Chamungu dk68, Matheo Anthony, Marcel Kaheza/ Henrico Kayombo dk72 na Jimmy Shoji/ Mohamed Mkopi dk89.

Post a Comment

0 Comments