Pamoja na kutengeneza nafasi nyingi dhidi ya Mbeya City jana, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema timu yake ilistahili kushinda lakini walipoteza nafasi nyingi
"Mimi kazi yangu ni kuwaelekeza wachezaji jinsi ya kutoa mpira nyuma na kuufikisha langoni kwa timu pinzani, kazi ya kufunga inabaki kwa wachezaji wenyewe," amesema
"Mchezaji hafundishwi na kocha kufanya maamuzi, ni jinsi akili yake itakavyo muelekeza"
Eymael amesema wanajitahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyopo kwani anapaswa kufanya kazi na wachezaji aliowakuta
"Mimi nilisajili mshambuliaji mmoja tu, Morrison, wanaosema safu yetu ya ushambuliaji ina mapungufu nafikiri mimi siwezi kuwa na majibu alipaswa kuulizwa kocha aliyepita"
"Napaswa kufanya kazi na wachezaji niliowakuta. Bahatimbaya hapa Tanzania hawaruhusu kusajili wachezaji huru kama sheria ya FIFA inavyoelekeza. Kwenye ligi nyingine mchezaji huru anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote hata wakati dirisha la usajili limefungwa"
0 Comments