Nahodha wa Simba John Bocco amesema ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Kagera Sugar, unaweka salama malengo yao ya kutetea ubingwa wa ligi kuu
Bao la dakika ya 61 lililofungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati, limeifanya Simba ifikishe alama 59 ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama 15
Simba ilitawala mchezo huo, mashabiki walitamani kuona idadi kubwa ya mabao inafungwa
"Lengo letu lilikuwa kuondoka na alama tatu, hilo tumelifanikisha. Tulitengeneza nafasi nyingi hata hivyo niwapongeze wapinzani wetu kwani nao walicheza vizuri na kuzuia mashambulizi yetu mengi"
"Tumeachana na matokeo hayo sasa tunajipanga na mchezo unaofuata"
Mabingwa hao watetezi wataelekea mkoani Mtwara kuifuata Ndanda Fc kwa ajili ya mchezo ambao utapigwa Jumapili
0 Comments