BETI NASI UTAJIRIKE

NCHIMBI ATOBOA SIRI YA USHINDI DHIDI YA MTIBWA

Mshambuliaji Ditram Nchimbi jana alitengeneza bao pekee la Yanga kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.Nchimbi aliingia kwenye kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrick Sibomanakrosi yake kutoka winga ya kulia ambayo ilizaa bao la kwanza lililowekwa kimiani na David Molinga 'Falcao'.Nchimbi ambaye hivi karibuni alikwenda Misri kufanya majaribio klabu ya Smouha, amesema ushindi waliopata jana ulitokana na mafanikio ya mpango wa kocha Luc Eymael kwenye kipindi cha pili

"Mwalimu alinipa maelekezo kutokana na mechi ilivyokuwa ikiendelea kwa sababu aliyekuwa akicheza winga alikuwa akicheza taratibu. Alinitaka nitumie nafasi iliyokuwa ikiachwa na walinzi wa pembeni wa Mtibwa Sugar ambao walikuwa wakipanda sana. Mwisho wa siku mpango wake umefanikiwa na tumeweza kushinda"

Nchimbi amewataka mashabiki wa Yanga waendelee kuwaunga mkono kwani timu imeanza kucheza vizuri na wachezaji wameongeza kujiamini.Wana matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwenye michezo inayofuata

Post a Comment

0 Comments