Mchezaji wa Simba SC Jonas Mkude amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United FC katika mchezo uliofanyika Februari 22, 2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Msemaji wa Timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari na kauli za maudhi kwa viongozi wa timu ya Polisi Tanzania FC katika mchezo uliochezwa Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro
Mchezo namba 233 (Polisi Tanzania vs Yanga SC) :
Waamuzi waliosimamia mchezo namba 223 Polisi Tanzania vs Yanga SC Abel Willium na Martin Mwalyaje wamefungiwa miezi mitatu (3) kwa kosa la waamuzi hao kushindwa kutafsiri sheria mchezo huo tajwa uliofanyika Februari 18, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.
Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 39(1A) ya Udhibiti wa Waamuzi.
Mchezaji na nahodha wa timu ya Yanga SC Papi Tshishimbi ametozwa faini ya Tsh. 200,000 (laki mbili) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano (interview) na mdhamini wa Ligi Kuu Azam Media katika mechi iliyofanyika Februari 23, 2020 uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga.Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa kanuni 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 232 - Polisi Tanzania FC 3 vs Ruvu Shooting FC 1 :
Timu ya Ruvu Shooting FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000.00 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kusababisha kutokea kwa vurugu zilizoongozwa na mwalimu wa timu hiyo Salum Mayanga pamoja na wachezaji wa timu hiyo,Shabani Kisiga, Emmanuel Martin na Rajabu Zahiri katika mchezo tajwa uliofanyika Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.
Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni 14(43) ya Ligi Kuu Kuhusu Taratibu za Mchezo.
Timu ya Ruvu Shooting FC waliomba marejeo (review) juu ya maamuzi yaliyotolewa na Kamati juu ya mchezo wao namba 205 dhidi ya Tanzania Prison FC ambapo timu hiyo ilipoteza mchezo kutokana na kutofata Kanuni ya 14(2l) ya Ligi Kuu.
Kamati ilipitia tena shauri hilo na maamuzi kubaki kama yalivyokuwa Ruvu Shooting FC kupoteza mchezo dhidi ya Tanzania Prison FC.
Mechi namba 240- Coastal Union 0 FC vs Yanga SC 0 :
Kocha wa Yanga Luc Eymael ametozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano (interview) na mdhamini wa Ligi Kuu Azam Media katika mechi iliyofanyika Februari 23, 2020 uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga. Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
0 Comments