BETI NASI UTAJIRIKE

MBRAZIL WA SIMBA MAJANGA MATUPU ,SVEN AKIRI KUTOMWELEWA

Mkufunzi wa Simba, Sven Vandenbroeck, anatambua kikosi chake kinakabiliwa na udhaifu kwenye safu ya ulinzi hasa mabeki wanaotakiwa kuwapokea Serge Wawa na Erasto Nyoni,


hivyo amepanga kuongeza sura mpya kabla ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Zaidi ya kuongeza mabeki wawili wa kati, Sven, anataka sura hizo mpya ziwe na uwezo mkubwa zaidi ya Wawa na Nyoni, akihitaji ushindani wa hali ya juu kwenye kikosi chake.
Benchi la Ufundi la Simba limeona na kukubali kwamba kuna uhitaji huo wa mabeki wa kati watakaokuwa bora zaidi ya waliopo hivi sasa ili kupunguza makosa mengi yanayotokea kwenye eneo hilo.
Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo, wamekuwa wakiwategemea zaidi Wawa na Nyoni katika kikosi cha kwanza.
Hata hivyo, linapokuja suala la kutoa nafasi kwa wengine, pia, kwa lengo la kuwapumzisha walinzi tegemeo, mambo huwa ni magumu kutokana na uhakika wa ulinzi kuwa ni mdogo.
Mbrazil, Tairone Santos na Kennedy Juma, ni mabeki ambao huwapokea Wawa na Nyoni katika michezo inayohitaji mabadiliko ya kikosi kwa ajili ya kuwapumzisha baadhi ya wanaoanza, lakini wameshindwa kuliridhisha benchi la ufundi hadi sasa.
Sven alikiri kuwepo kwa udhaifu huo katika safu yake ya ulinzi hasa wanapokosekana mabeki wake tegemeo, lakini aliweka wazi kwamba takribani vijana wake wote wamekuwa wakijituma kuhakikisha wanaisaidia Simba msimu huu.
"Safu ya ulinzi huonyesha ubora wanapokuwepo wachezaji fulani, lakini wakikosekana kunatokea makosa mengi mno, itabidi tupate mabeki wengine wawili watakokuwa bora zaidi ya waliopo hivi sasa.
"Nilitaka kuwatumia wachezaji wote ambao sijawapa nafasi katika michezo ya hivi karibuni, lakini wameshindwa kutimiza majukumu kikamilifu na kuufanya mchezo kuwa mgumu.
"Kwa sababu tunataka kuwa na timu itakayokuwa na ushindani nikiendelea kuwepo. Katika usajili ujao, jambo la kwanza kuanza nalo ni suala la kupata beki bora zaidi ambao wataleta ushindani," alisema.
Kauli hiyo ya Sven juu ya kufanya usajili wa mabeki wapya ni baada ya Mbrazil, Santos, kufanya uzembe uliosababisha wapinzani wao kwenye mchezo wa Kombe la ASFC (Azam Sports Federation Cup), Stand United, kupata bao la kusawazisha.
Katika mchezo huo uliochezwa juzi mkoani Shinyanga, Simba walipata bao la kwanza kupitia kwa Hassan Dilunga, kabla ya Miraji Salehe kuipa bao la kusawazisha Stand United. Salehe alitumia uzembe wa Santos kukosa utulivu akiwa karibu na mstari wa kati wa uwanja.
Katika changamoto ya mikwaju ya penalti, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 3-2.

Post a Comment

0 Comments