BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA ATUMA UJUMBE MZITO KUELEKEA MCHEZO NA MTIBWA SUGAR LEO

Mabingwa wa nchi Simba leo wako mkoani Morogoro kuwakabili wana tamtam wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri.Huu ni mchezo muhimu sana kwa Simba pengine kuliko wapinzani wao Mtibwa Sugar licha ya kuwa nao wako katika presha ya kupata matokeo baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo.Jana kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alibainisha waziwazi kuwa leo wanahitaji kupata ushindi bila ya kujali mazingira yoyote watakayokutana nayo

Matokeo ya kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania hayakuwafurahisha Wanamsimbazi, hivyo leo hakuna matokeo mengine ambayo yanaweza kurejesha amani ya mashabiki zaidi ya ushindi
Msemaji wa Simba Haji Manara amewahasisha wachezaji kuwa leo wafahamu umuhimu wa kupata matokeo mkoani Morogoro

"Najua mnajua nini Wanasimba wanataka leo?. Najua mnajua Washabiki wetu watakuwa ktk hali gani jioni ya leo bila ushindi!!

Najua mnajua msingetamani nife au niumwe kisa matokeo mabovu leo. Mimi na Wanasimba wote tunawaamini na tunajua mkipambana hakuna wa kuwafunga nyie"
"Tuleteeni pointi tatu leo, nendeni kachezeni kwa spirit kubwa ili mwishoe tuondoke vinara uwanjani!!
Mungu wabariki Wafalme Simba, Mungu wape nguvu Machampioni wa nchi, wape na Maarifa wachezaji wetu wapendwa Insha'Allah"

Post a Comment

0 Comments