BETI NASI UTAJIRIKE

KIBOKO YA HAJI MANARA AREJEA JANGWANI KUMKABILI MECHI YA WATANI

Aliyekuwa msemaji wa Yanga na Sasa ni mkuu wa wilaya ya Arumeru amerejea tena mitaa ya Jangwani kuelekea michezo ya ligi na kombe la FA dhidi ya gwambia na ule wa tarehe 8 Machi dhidi ya Simba 


Jerry Muro akiwa klabuni hapo alinukuliwa akisema 

" Nipo hapa kuwatangazia wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa jumla kuwa  huu ndio muda rasmi wa Yanga, ile kampa kampa tena inarudi. . Password tunazo sisi na tayari nishampa katibu na kocha wetu . .Tutapambana na yeyote anayetaka kuionea ama kuidhurumu. .  Yanga Viongozi mliokuwepo rudini tuungane , mimi nimekuja hakuna aliyeniita nimeona fedheha ,karaha zimezidi. . Ukuu wa wilaya ulinikuta nikiwa Yanga SC . . Usisubiri kuitwa wala kuchaguliwa katika kamati kama unaumia na Yanga njoo. . Mkemi, Kleb na wengineo tunajuana wale wazee wa kamati ya miba. .Njooeni tusikae pembeni kulalamika, njoeni tuungane milango ipo wazi viongozi nishaongea nao hawana hiyana na hawawezi mzuia mtu. . 

"Uongozi ni kupokezana vijiti, nimeondoka nimewaachia akina Nugaz, kuna ndugu yangu yupo tu ameng'ang'ania kama kigando au ni msukule wa Simba ? au hana kazi nyingine ya kufanya? rudi kafundishe madrasa maana ndio elimu pekee uliyonayo. . na akiongea ongea ovyo asisahau kuwa mi mkuu wa wilaya ntamuweka ndani masaa 48"

Jerry Murro.

Post a Comment

0 Comments