BETI NASI UTAJIRIKE

KAULI ZA JERRY MURO ZAIBUA SINTOFAHAMU NDANI YA YANGA

Kauli ya aliyekuwa msemaji na mhamasishaji wa Klabu ya Yanga mheshimiwa Jery Muro imeibua mtafaruku miongoni mwa Mashabiki wa Yanga


"Nimesikitishwa sana na maneno ya Jerry Murro alipokuwa akihojiwa na Wasafi FM katika kipindi chao kiitwacho Sports Arena asubuhi ya leo.

Jerry amewaponda na kuwakebehi baadhi ya wachezaji wetu akifikia hatua ya kuwaita Boya, amemkebehi mwalimu wetu Luc Eymael na kumpigia chapuo Boniface Mkwasa, ameamsha vuguvugu juu ya udhamini wetu kutoka GSM akitaka turudi kwenye kuchanga buku buku tena na amejinasibu kuwa wao ndio watakaopanga kikosi siku ye leo.

Kupitia maneno yake sio siri tena kuna baadhi ya mambo yamefichuka na Adui wa Yanga ni mwana Yanga mwenyewe, na kuna mvutano katika benchi la ufundi kati ya Mkwasa na Luc. . ikishindikana itabidi Mkwasa aondoke! Pia utaratibu wa utoaji pesa kutoka GSM hauwafurahishi viongozi wengi pale klabuni kwa maana hakuna mianya ya upigaji hivyo kuna zengwe linaendeshwa.

Jerry tulitegemea utaongelea maovu ya TFF dhidi ya klabu yetu, utaamsha ari ya umoja na hamasa kwa wana Yanga wote lakini imekuwa tofauti. .

Tusiwe wepesi wa kusahau na kumkumbatia sana Murro, Yeye ni mmojawapo waliompiga vita Manji, yeye ni mmoja wapo walioiponda Yanga kipindi tunapitia magumu leo kuna afadhali anarejea tena kwa kisingizio yupo likizo. Jana alisisitiza mwana Yanga yeyote ukiwa na dukuduku ama tatizo kawasilishe mawazo yako klabuni, iweje leo yeye dukuduku lake alitoe katika vyombo vya habari? leo ataongea na wachezaji wetu vipi wale aliowatukana watakuwa katika ari ipi?Ngass, Kaseke, Molinga, Yikpe watajisikiaje? vipi kuhusu kocha wetu Luc atajisikiaje?Jerry ameharibu morali ya timu yetu na kuleta mpasuko au mpango wake huu una baraka za viongozi wa Yanga ?

Wana Yanga SC tupo pamoja na GSM daima!"

Nini maoni yako kuhusu Jerry Muro na mapendekezo yake kuhusiana na Yanga hasa wanapojiandaa na Mchezo wa FA dhidi ya gwambina fc na ule wa ligi dhidi ya Simba tarehe 8 machi?

Post a Comment

0 Comments