BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAELEZEA KINACHOPELEKEA WAKAPATA SARE 4 MFULULIZO

Hakuna shabiki wa Yanga anayeweza kufurahia mwenendo wa timu wakati huu, sare tatu mfululizo sio matokeo ya kufurahiwaWengi wametoa maoni yao kwa kile ambacho wanadhani kikifanyiwa kazi na benchi la ufundi, manufaa yanaweza kupatikana


Benchi la ufundi lina nafasi ya kuchambua na kufanyia kazi yale ambayo wengi wanadhani inafaa yarekebishwe.Maoni mengi yametolewa, baadhi yake ni haya;

1. SAFU YA ULINZI
Kumekuwa na mtazamo tofauti kuhusu safu ya ulinzi wa Yanga, hasa pacha ya walinzi wa kati
Wakati Lamine Moro akicheza sambamba na Said Juma Makapu huku mlinda lango akiwa Metacha Mnata, Yanga iliweza kucheza takribani mechi tatu bila ya kuruhusu bao
Lakini pacha ya Shikhalo, Lamine na Yondani imekuwa ikiruhusu mabao mara kwa mara
Wapo wanaohoji Andrew Vicent na Ally Ally kwa nini hawapewi nafasi?
Ukizungumzia mabeki mahiri wa kucheza mipira ya juu kwenye kikosi cha Yanga ni Lamine Moro, Andrew Vicent na Ally Ally
Yanga ilisitisha mpango wa kumtoa kwa mkopo Ally Ally lakini haonekani kuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza

2. Mfumo wa 4-4-2 unaweza kuwa bora
Kocha Luc Eymael anapendelea zaidi mfumo wa 4-2-3-1 ambapo anatumia mshambuliaji mmoja mbele
Hata hivyo Yanga haionekani kufunga mabao mengi kupitia mfumo huo
Msimu huu imefunga mabao 25 na kuruhusu mabao 18, wastani wa chini sana kuonekana kwenye miaka ya karibuni
Pengine kuanza na washambuliaji wawili inaweza kuwa na manufaa
David Molinga, Tariq Seif na Ditram Nchimbi wanaweza kupokezana nafasi mbili za ushambuliaji huku Patrick Sibomana, Deus Kaseke na Mrisho Ngasa wakarejeshwa majukumu ya ushambuliaji wa kutokea pembeni
Eymael anamtumia Nchimbi winga ya kulia hivyo kumuondoa kikosi cha kwanza Patrick Sibomana ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji tegemeo wakati wa Zahera na Mkwasa

3. Patrick Kabamba haonekani
Wakati wa dirisha dogo Yanga ilimsajili winga Patrick Kabamba kutoka klabu ya Buildcon Fc ya nchini Zambia
Kabamba alisajiliwa baada ya kufuzu majaribio
Hata hivyo mchezaji huyo bado hajaonekana kikosini wengi wakiwa na shauku ya kumuona akipewa nafasi

4. Yikpe bado
Ukweli ni kwamba mshambuliaji Yikpe Gnamien ameshindwa kuwashawishi Wanayanga licha ya kuwa amefunga mabao mawili tangu asajiliwe dirisha dogo
Eymael ana imani kuwa mshambuliaji huyo atakuwa sawa, lakini uvumilivu umeanza kuwashinda mashabiki
Mbelgiji huyo amekiri Yikpe raia wa Ivory Coast kuwa na mapungufu huku akiahidi kumsaidia

Post a Comment

0 Comments