BETI NASI UTAJIRIKE

GSM WATOA WARAKA MZITO UWEKEZAJI NDANI YA YANGA

Yanga ilitangaza kamati ambayo itasimamia na kuiongoza Yanga SC kuelekea mfumo wa kisasa, sisi kama GSM pamoja na kuwa na plan nyingi za kusaidia timu in terms of technical bench na wachezaji ambazo tayari tumezifanya kwa kiasi kikubwa


 Juzi tumemleta pia mtaalamu mwingine kutoka south Afrika ambaye ataongezeka katika technical bench kuungana na Luc, Riedoh. Hii yote ni kuifanya Yanga SC kuwa na nguvu,".
"Tunaendelea na tutaendelea kufanya vitu vingine ambavyo vipo nje ya mkataba , lengo ni kuendelea kuisaidia timu yetu ya Yanga SC,".


"Tukizungumzia kambi ambayo timu inakaa na uwanja wa kufanyia mazoezi ni 100% GSM inasimamia,".
Tukaona haitoshi tu kuona timu ya Yanga inafanya vizuri uwanjani, tukaona tuwasaidie kuwapeleka katika mfumo ambao klabu itakuwa imara,".

"Watu wengi wanaweza wakadhani GSM ina nia ya kuichukua Yanga, ama kuimiliki. . hapana sisi lengo letu ni kuisaidia Yanga SC,"Kamati iliyoundwa kusimamia mabadiliko  ina watu weledi sana, lakini changamoto wengi hawawezi kujitolea 100% kusimamia mchakato huo kwa kuwa wamebanwa na majukumu mengine ikizingatiwa mabadiliko yanahitajika haraka sana,". 

"Kwa kuliona hilo ndio maana tukamleta mtaalam Antonio Pinto ambaye ana experience kubwa sana kutokea Benfica na atakuwa dedicated katika wajibu huo. na amefanya mambo makubwa sana Benfica, ambapo wameuza wachezaji wenye thamani ya euro milioni 600 katika kipindi cha miaka 10, na wametwaa ubingwa mara 8 katika miaka 10,".


"Huyu hajaja katika operation za Yanga, amekuja katika transformation project tunayoitarajia kuifanya kama klabu,".Pinto anaondoka leo, amekuja kwa ajili ya makubaliano na majadiliano ambayo tayari tumeafikiana,". 


"Sisi GSM tumefanya miradi mingi sana ambayo haijawahi kufail na ipo very succesfull na huu mradi nakuhakikishia utakuwa very succesful,". Hatutaendana na zile njia ambazo watu wanazitumia. .tutakwenda very profesional tutampa muda Pinto nakuhakikisha ana fikia malengo. . hii project team itaenda bega kwa bega na kamati ya mabadiliko ya klabu ili kuhakikisha tunaendana na matakwa halisi ya nchi yetu,". 


"Pia tutafanya mabadiliko ya katiba ili kuendana na mabadiliko tunayoenda kufanya, hivi vitu vyote vitaenda parallel"Muelekeo wetu ni kuisaidia Yanga SC isimame kwa miguu yake miwili,". 


"Infrastructure kuna trainning facility, sehemu ya kulala wachezaji na kuhakikisha viongozi wanakuwa na ofisi nzuri na zenye hadhi. . muda mfupi tu nawahakikishia kila kitu kitabadilika Yanga SC na itakuwa ni klabu yenye mafanikio makubwa kuliko klabu yoyote ukanda wa Afrika mashariki na kati,".

Post a Comment

0 Comments