BETI NASI UTAJIRIKE

FRAGA AMPOTEZA MORRISON VIJIWE VYA KAHAWA

Mashabiki wa Simba ambao juzi walijitokeza katika Uwanja wa Taifa, Dar, walikuwa na kazi moja tu ya kuwajibu wenzao wa Yanga kuwa ‘Nyie mna Mghana, sisi tuna Mbrazili mabao.’


Jeuri hiyo ya mashabiki hao waliipata baada ya kiungo wao, Gerson Fraga raia wa Brazil kufunga mabao mawili na kuwapa pointi tatu  Simba mbele ya Coastal Union.

Kiungo huyo kwa mara ya kwanza aliibuka tena katika kikosi cha kwanza cha Simba baada ya kuzikosa mechi sita mfululizo na kuja kuibuka shujaa kwa kufunga mabao hayo katika ushindi walioupata wa mabao 2-0.

Fraga alifunga bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi ya Clatous Chama dakika ya saba kipindi cha kwanza. Mbrazili huyo aliihakikishia Simba pointi tatu baada ya kuweka bao la pili akimalizia kirahisi mpira uliopigwa na Hassan Dilunga dakika ya 78 na kuifanya Simba kuibuka kifua mbele.

Kwa upande wa vijiwe vya kahawa Mbrazil huyo amekuwa gumzo kutokana na uwezo mkubwa anaokuwa anauonyesha mara zote anapopata nafasi ya kucheza. Mashabiki hawataki kumzungumzia Morrison kutokana na kupotezwa na Humudi  kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa huku akishindwa kuonyesha mbwembwe zozote kwenya mchezo huo

Kwa sasa Simba wanazidi kukaa kileleni wakiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 18 na kushinda mechi 15, huku wakiiacha Yanga pointi 19 ikiwa imecheza mechi 15.

Post a Comment

0 Comments