BETI NASI UTAJIRIKE

FAHAMU MICHEZO 9 ZITAKAZOPIGWA LEO LIGI KUU BARA

Ligi kuu Tanzania bara inaendelea tena leo kwa michezo 9 itakayozikutanisha timu 18 zinazoshiriki michuano hiyo. Klabu za Simba,Yanga ,Azam na Mtibwa ni moja ya timu zitakazotazamwa zaidi kwa leoMechi Tatu bora kwa leo

Mtibwa Sugar vs Simba 

Mchezo huu utapigwa mkoani morogoro majira ya saa 10:00 alasiri dimba la Jamhuri na ni mchezo utakaotazamwa zaidi kutokana na ushindani na tambo za timu hizo mbili. Kocha wa Simba atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha anashinda mchezo hu ili kunusuru kibarua chake wakati huo huo atakuwa na kazi ya kulipa kisasi cha kufungwa na Mtibwa michuano ya kombe la mapinduzi. Upande wa Mtibwa wao wanamalengo ya kutopoteza mchezo huo baada ya kupoteza ule wa Yanga na wamedhamilia kuucheza mchezo huo kwa nguvu zote

Azam FC vs Polisi Tanzania

Ili vijana wa Bakhresa waweze kubaki nafasi ya pili na pengine kuongoza katika ligi kuu Tanzania bara basi wanapaswa kuifunga Polisi Tanzania. Mchezo huo utapigwa dimba la Uhuru majira ya saa 10 jioni na utaaonyeswa katika Runinga.

Yanga Vs Mbeya City

Yanga wapo nyuma ya Simba kwa pointi 13 ,wanalazimika kucheza kwa juhudi zaidi ili  kuweza kupanda mpaka nafasi ya pili iliyokaliwa na Azam FC. Mchezo wa Yanga wakimkaribisha Mbeya City utapigwa saa 01:00 usiku na wakati huo huo Yanga atalazimika kushinda ili asherehekee miaka 85 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Hii hapa ratiba nzima ya michezo hiyo


Post a Comment

0 Comments