BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AHITAJI MIUJIZA KUWANG'OA SIMBA KILELENI

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji amefunguka kuwa ana uhakika mkubwa wa timu yake kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu bara msimu huu kutokana na kuonekana kwa mabadiliko kwenye kikosi chake.


Kabla ya matokeo ya mchezo wa leo, Yanga inakuwa imepitwa pointi 13 na vinara Simba ambao wana alama 50 wakati wao Yanga wanazo 37 wakiwa nafasi ya tatu.Eymael alisema:

 “Kikubwa ambacho nakiona, ni kwamba timu yangu imebadilika kwa kiwango kikubwa na kadiri siku zinavyokwenda ndiyo inazidi kuwa bora, naamini nafasi ya ubingwa tunayo tena kubwa.

“Binafsi sina presha juu ya hilo na wala hatupaswi kuogopa kwamba nani anaongoza ligi kwa lengo la kukata tamaa, jambo kubwa ni kuendelea kupigana kuona kwanza tunawapita wapinzani wetu ili kuweza kufikia ubingwa kitu ambacho bado kipo kwenye uwezo wetu.

Post a Comment

0 Comments