BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AFUNGUKA TETESI ZA KUTIMULIWA YANGA

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kushangazwa na taarifa zinaodai kuwa ameomba kuvunja mkataba wake Yanga kurejea Afrika Kusini baada ya kuchukizwa na mwenendo wa uendeshwaji wa ligi kuu ya Tanzania Bara


Eymael amesema walioanzisha uvumi huo wana lengo la kumgombanisha na waajiri wake, klabu ya Yanga
"Hawa watu walioeneza uongo huu hawana nia njema nami, nafikiria kuwachukulia hatua kwani wananichonganisha na waajiri wangu," alisema Eymael
Kocha huyo raia wa Ubelgiji baadae leo ataiongoza Yanga kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Gwambina Fc ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakakebela alisema Eymael ataendelea kuwepo Yanga kwani ana mkataba wa miezi 18
"Eymael ni kocha wetu, tutaendelea kuwa nae kulingana na makubaliano ya mkataba tulioingia," alisema
Eymael alisaini mkataba wa miezi 18 kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Post a Comment

0 Comments