BETI NASI UTAJIRIKE

BUMBULI ATANGAZA VITA KWA WAPINZANI WA YANGA

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baada ya kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la FA,


 wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo yote inayofuata
Kesho Jumamosi Yanga itashuka kwenye uwanja wa Uhuru kumenyana na Alliance Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Bumbuli amesema presha ya kukosa matokeo mechi zilizopita imemalizika baada ya kuifunga Gwambina Fc
"Mechi chache nyuma tulikuwa kwenye presha ya kupata matokeo, lakini baada ya ushindi dhidi ya Gwambina, tutaendelea kugawa vipigo kwa kila anayekuja mbele yetu"
"Tunawapa ujumbe wapinzani wetu kuwa sasa tuko tayari, kila anayekuja mbele yetu ajipange kwelikweli. Wale waliokuwa wanasema tunaihofia Gwambina, wajue hili, hatuhofii timu yoyote hapa Tanzania, wao wanaokuja kucheza nasi ndio wanatuhofia," amesema Bumbuli
Yanga itacheza mechi mbili dhidi ya Alliance Fc na Mbao Fc kabla ya mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa March 08 uwanja wa Taifa

Post a Comment

0 Comments