BETI NASI UTAJIRIKE

NYOTA WA YANGA AREJEA RASMI DIMBANI

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kukosekana dimbani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu akiuguza majeraha ya gotiMchezo wa mwisho ambao Mahadhi alishiriki ni wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ambao ulipigwa August 18 2018 kwenye uwanja wa Taifa
Ni katika mchezo huo ambao Mahadhi alipata majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa muda mrefu

Winga huyo mwenye kasi ya kimbunga, alifanyiwa upasuaji wa goti mara mbili, akipata matibabu ya kwanza Hospitali ya Muhimbili kabla ya kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi


Ni jambo jema kuona leo amerejea uwanjani, bila shaka ataweza kurejesha makali yake na kutoa mchango wake Yanga

Post a Comment

0 Comments