Mshambuliaji wa Aston Villa Mbwana Samatta amewaomba mashabiki wa soka nchini kuacha kutukana kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu yake hiyo pamoja na kurasa za wachezaji wenzake
Samatta amekuwa mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza ligi kuu ya Uingereza huku akifanikiwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza mwishoni mwa wiki dhidi ya Bournemouth
Hata hivyo kumejitokeza mashabiki Watanzania ambao wameingia kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya baadhi ya wachezaji wa Aston Villa wakiwatuhumu kumnyima pasi nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania.Samatta ameeleza kutofurahishwa na kitendo hicho akiwasihi waache tabia hiyo
Naye Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa soka nchini kuacha tabia hiyo kwani wanaweza kumharibia Samatta
"Watanzania nawasihi sana kama mnampenda Samata na kumtakia kheri katika maisha yake huko Aston Villa,tuache kutukana na kuongea maneno ya hovyo kwa wachezaji wenzie na klabu yake kwa ujumla!!"
"Msidhani kufanya hvyo ndio kumpenda Champion boy,ni kumweka katika presha ambayo hastahiki kwa sasa,Mnakosea sana na sasa tuanze kukemeana huu upuuzi tunaoupeleka kule"
"Grealish hawezi kumnyima pasi Samata kusudi kwa sababu yoyote ile,,level ya professional player hawafanyi ujinga ujinga huo,,na kuendelea kumtukana Nyota huyo wa Villa na captain wao ni kumweka mwenzetu katika hali ngumu klabuni!!"
"Kiukweli tunafanya ushamba mkubwa na inaonyesha ulimbukeni wetu Wabongo Kiufupi social media hatuitendei haki Watanzania wengi na hz Abuse kwa wazungu msidhani wanachukulia tunavyochukulia sie,mnaotutukana kila siku!!"
"Wote tushiriki kumsaidia mchezaji wetu bila kumtengenezea mazingira magumu katika kazi yake inayoitangaza nchi"
0 Comments