BETI NASI UTAJIRIKE

KWA KOMBINESHENI YA EYMAEL NA MKWASA HATOKI MTU AISEE

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael alianza majukumu yake vibaya kwenye kikosi cha Yanga akipoteza michezo yake yote miwili ya kwanza


Hali hiyo ilipelekea kuibuka kwa sintofahamu kwenye benchi la ufundi ambapo kwa nyakati tofauti ilielezwa Eymael alipendekeza aletewe kocha mwingine msaidizi badala ya Charles Mkwasa aliyekuwa pendekezo la uongozi wa Yanga

Hata hivyo sasa inaelezwa Eymael ameridhia kufanya kazi na Mkwasa baada ya kujiridhisha kuwa anahitaji uzoefu wa nguli huyo wa klabu ya Yanga.Kabla ya uamuzi huo, uongozi wa Yanga ulikuwa mbioni kumalizana na mkufunzi wa Kagera Sugar Meckie Mexime

Chini ya Eymael na Mkwasa, Yanga sasa imeshinda michezo mitatu mfululizo tangu walipopoteza michezo miwili ya kwanza.Jambo jema zaidi, kiwango cha mabingwa hao wa kihistoria kimeendelea kuimarika siku hadi siku jambo linalowapa furaha mashabiki

Mkwasa alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga kwa muda baada ya uongozi wa timu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha mkuu, Mwinyi Zahera mwezi Novemba 2019.Yanga haikupoteza mchezo wowote katika kipindi chote ambacho ilikuwa chini ya Mkwasa

Post a Comment

0 Comments