BETI NASI UTAJIRIKE

BUMBULI AENDELEA KURUSHA VIJEMBE KWA TFF

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema TFF ilipaswa kumchukulia hatua Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto kufuatia kauli yake ya kuisahau Yanga kuipangia ratiba ya mechi zake


Akihojiwa na chombo kimoja cha habari mapema leo, Bumbuli alisema ni jambo lisilowezekana kuisahau klabu ya Yanga kutokana na historia yake

"Wale waliomuhoji kiongozi wa Bodi ya ligi halafu akasema wameisahau Yanga, ilipaswa wamchukue wampeleke Hospitalini kumchunguza kwani sidhani kama alikuwa sawa," alisema Bumbuli

"Haiwezekani kiongozi wa mpira nchini leo hii useme umeisahau Yanga, timu yenye historia kubwa zaidi kwenye soka la Tanzania"

"Unapozungumzia Yanga, unazungumzia mabingwa wa kihistoria wa soka la Tanzania. Sasa ukiona kiongozi anatoa kauli kama ile fahamu kuna shida"

Post a Comment

0 Comments