Baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, leo Yanga ina nafasi ya kurekebisha makosa itakapochuana na Azam Fc katika mchezo
utapigwa uwanja wa Taifa saa moja jioni
Ni mchezo ambao matokeo tofauti na ushindi yanaweza kumuweka kwenye presha mapema kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael
Lakini pia ni mchezo ambao vijana wa Eymael wanahitaji kuongeza umakini ili kuweza kupata matokeo kwani Azam Fc ni moja ya timu bora kwenye ligi msimu huu
Washambuliaji David Molinga na Tariq Seif pamoja na kiungo nahodha Papy Tshishimbi wanatarajiwa kuongeza nguvu Yanga baada ya kurejea kikosini
Yanga pia imewaongeza mawinga Patrick Kabamba na Bernard Morrison ambao inaelezwa vibali vyao viko tayari.Hata hivyo Morrison alijiunga na timu jana, atahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi na wenzake
Leo Eymael huenda akafanya mabadiliko ya kikosi alichokitumia mchezo dhidi ya Kagera Sugar
0 Comments