BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA,COASTAL UNION,NJOMBE MJI ,MKAMBA RANGERS NA PRISONS ZAPIGWA RUNGU NA TFF

Uongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti Msolla Mshindo umeonekana kuwa na nidhamu mbovu kuanzia mashabiki  ,wachezaji na makocha waliowahi na wanaoifundisha timu hiyo. Leo Asubuhi TFF imebainisha makosa 


ya vilabu mbalimbali ikiwemo Yanga waliokutwa na makosa manne, Prisons ,Njombe mji na Mkamba rangers,Costal Union

Adhabu kwa Mkamba rangers 
Mechi namba 18A: Mkamba Rangers 1 vs Villa Squard 0-Klabu ya Mkamba Rangers imepoteza mchezo dhidi ya timu ya Villa Squard baada ya timu hiyo kufanya udanganyifu wa Leseni kwa kubandika picha(sura) za wachezaji wengine katika ;leseni halali zilizotolewa na TFF. Mchezo huo uliyofanyika Disemba 10,2019 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi Daraja la Pili namba 43(23) kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Hivyo timu ya Villa Squard imepewa pointi tatu na magoli matatu katika mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni namba 14(36) kuhusu Taratibu za Mchezo
Vile vile viongozi wa Tiimu ya Mkamba Rangers Katibu(Bw.Azizi Mfayeka), Timu Meneja(Kelvin John) na Kocha(Rashid Tuli) wamepelekwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kitendo cha Udanganyifu wa leseni za wachezaji.
Pia Kamishina wa mchezo huo Bw Laurent Chacha amepelekwa katika Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).

Adhabu kwa njombe mji 
Timu ya Njombe Mji imepoteza mchezo dhidi ya Friends Rangers baada ya kuwa na wachezaji pungufu ya saba(7) katika mechi iliyofanyika Januari 19,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.Hivyo timu pinzani imepewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni namba 14(37) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo

Adhabu kwa Coastal Union
Mjumbe wa Kamato ya Utendaji wa Klabu ya Coastal Union Bw Salum Perembo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kutaka kuingia uwanjani kwa lengo la kuwashambulia waamuzi huku akitoa maneno makali katika mechi iliyofanyika Januari 11.2020 katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Adhabu kwa Yanga 
Klabu ya Yanga Sc imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na pia wakati wa mapumzikokwenye mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Januari 04 2020.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamati ya TFF ya saa 72, mashabiki hao pia waliwarushia chupa za maji waamuzi wakati wanaelekea vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Adhabu Kwa Yanga 
Vile vile katika mchezo huo Klabu ya Yanga Sc imepigwa Faini ya Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kutokutumia chumba rasmi kilichoandaliwa kwa kubadilishia nguo.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Adhabu kwa Yanga na Prisons 
Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga Sc zimepigwa Faini ya Tsh.500,000/=(Laki Tano) kila mmoja kwa kosa la kutokuwakilisha vikosi vya timu zao kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo katika mechi hiyo iliyochezwa Disemba 29,2019 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Adhabu dhidi ya Timu hizo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.


Adhabu kwa Kocha wa Yanga 
Kocha wa Klabu ya Yanga amepewa Onyo kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa na Klabu ya Yanga imeelekezwa kumuelimisha kocha wao na kusimamia nidhamu kwa ujumla..



Post a Comment

0 Comments