Mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kumaliza utata wa nani mbabe kwa mwaka 2020 kati ya watani wa Jadi, Simba na Yanga ilimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili.
Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Medie Kagere dakika ya 42 baada kushikiliwa na Kelvin Yondani ndani ya boksi, bao ambalo limedumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Mara tu baada ya Kipindi cha pili kuanza, dakika ya 46 tu Deo Kanda akaiandikia Simba goli la pili, hali ambayo iliwalazimu Yanga kufunguka na kusaka bao kwa udi na uvumba.
Dakika tatu tu baadaye, Mapinduzi Balama akaiandikia Yanga bao la kwanza huku Banka akiiandikia yanga bao la pili na la kusawadhisha kunako dakika 53.Hadi dakika 90 zinamalizika, Simba 2-2 Yanga.
0 Comments