BETI NASI UTAJIRIKE

UONGOZI YANGA WATOA NENO BAADA YA EYMAEL KUONYWA NA TFF

Baada ya Kocha wao Mkuu, Luc Aymael, kupewa onyo kutokana na kauli ya kusema alifanyiwa ubaguzi, uongozi wa klabu hiyo umesema hauna namna ya kupingana na maamuzi ya kamati ya saa 72.


Katika mechi ya ligi ambayo Yanga walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Azam, Luc Aymael alilalamikia suala la Mwamuzi, Hance Mabena kukataa kumpa mkono baada ya kupewa kadi ya njano.

Aymael alipewa kadi hiyo kufuatia malalamiko aliyokuwa akiyatoa wakati mchezo huo unaendelea katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema wao kama Yanga wamepokea onyo hilo na hawawezi kulizungumzia  na wamelipokea kwa mikoni miwili.

"Unajua kauli ama maamuzi yakishatoka hata kama ni onyo hauwezi kupingana nalo, sisi tumelipokea na hatuwezi kupingana nalo wala kuongeza chochote."

Post a Comment

0 Comments