BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WASHINDWE WAO TU ILA SINGIDA WANAFUNGIKA KIRAHISI

Kikosi cha Yanga kiko mkoani Singida ambapo jioni ya leo watashuka katika dimba la Namfua kuikabili Singida United ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.Yanga ilitua Singida juzi jioni 


jana ikapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Namfua ambao leo utatumika kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa maboresho.Baada ya mfululizo wa kukosa ushindi katika michezo mitatu iliyopita, mchezo wa leo Yanga haihitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi.

Wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na hata mashabiki leo watakuwa na siku mbaya sana kama mambo hayatabadilika.Mkufunzi wa mabingwa hao wa kihistoria Luc Eymael amesema wamerekebisha baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwenye michezo iliyopita hivyo leo wana kila sababu ya kushinda

Eymal bado hajaonja radha ya ushindi tangu atue Yanga wiki mbili ziliyopita .Mchezo utapigwa saa kumi kamili jioni

Post a Comment

0 Comments