Kikosi cha Yanga leo saa mbili na robo usiku kitaana kampeni zake za kuwania ubingwa wa kombe la mapinduzi dhidi ya Jamhuri. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Amaan.
Klabu za Azam na Mtibwa Sugar zimeshafuzu hatua ya nusu fainali baada ya hapo jana kushinda michezo yao ya robo fainali huku Yanga na Simba zikitegemewa kufuzu hatua hiyo hii leo.
Kama Yanga akishinda mchezo wa leo dhidi ya Jamhuri basi atacheza na Mtibwa Sugar hatua ya nusu fainali. Na kama Simba itaifunga Zimamoto basi timu hiyo itakutana na Azam FC hatua ya nusu fainali.
Kama Yanga na Simba zitashinda michezo yao ya nus fainali basi timu hizo zitacheza fainali. kama timu hizo zitatolewa hatua ya nusu fainali basi zitakutana kwenye kinyang'anyilo cha nafasi ya 3
0 Comments