BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA: KAMA MKWASA TU MMEMSHINDWA JE LUC EYMAEL MTAMUWEZA?

Klabu ya Yanga imemtangaza kocha mpya anayehukua nafasi ya Mwinyi Zahera iliyokuwa inakaimiwa na Kocha mzawa Boniface Mkwasa. Mkwasa alipewa nafasi ya kuiongoza Yanga kwa kipindi cha miezi miwili baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera 


kutimuliwa klabuni hapo. Mkwasa ameiongoza Yanga kwa mafanikio makubwa na alifanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bor mwezi Disemba. Mkwasa pia alifanikiwa kuiongoza Yanga kwenye mechi dhidi ya Simba kwa kupata sare ya mabao 2-2 akitokea nyuma.

Klabu ya Yanga imemtangaza Luc kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na sasa ataiongoza Yanga mpaka mwishoni mwa msimu huku akiwa na mechi 21 za kuonyesha uwezo wake. Hii ni CV ya Kocha Luc Eymael.

Akiwa na AS VITA
🏆 Ligi kuu DR Congo - 2010
🏆 Super Coupe du Congo - 2010

Akiwa na Missile ya Gabon
🏆 Chhampionnat National D1 - 2010–11

Akiwa A.F.C. Leopards - Kenya
🏆 Nafasi ya pili -2013
🏆 FKF President's Cup - 2013

Akiwa Rayon Sports Rwanda

🏆Nafasi ya pili 2013–14

Akiwa na Free State Stars - Afrika
🏆Nedbank Cup - 2018

P
ia huyu alikuwa mchezaji enzi zake alicheza takribani michezo 729 Kwa miaka 25 Kuanzia mwanza 1975-2000.


Amehudumu kama kocha kwa miaka 20 (1999-2000). Ana leseni ya Uefa Pro aliyopata 2007 na uefa A aliipata mwaka 2002.

MAFANIKIO YA KIBABE ALIYOWAHI KUFANYA

Aliisaidia Missile kunyakua ubingwa wa kwanza kabisa katika historia yao. Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 2003.

Alitua AFC Leopard mwezi April 2013 akaikuta klabu hiyo nafasi ya mwisho. Kufikia August 2014 alimaliza nafasi ya 2 na klabu hiyo. Akabeba kombe la raisi na kusaidia klabu hiyo kucheza kombe la shirikisho.

Aliipeleka JS Kairouan nafasi 8 ambayo ilikuwa kwa mara ya kwanza klabu hiyo kumaliza nafasi ya juu kama hiyo.

 Aliipeleka Polokwane City nafasi ya 5 ambayo ilikuwa kwa mara kwanza klabu hiyo kufika nafasi za juu kama hiyo.

Eymael aliisaidia Free State kunyakua kombe la kwanza katika kipindi cha miaka 24 tena kwa kuwatungua Kaizer Chiefs 2-0 nusu fainali ya Nedbank Cup.

Post a Comment

0 Comments