Hiyo imekuja kufuatia mwekezaji huyo kuamua kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, muda mfupi baada ya Simba kufungwa na Mtibwa Sugar katika fainali ya Mapinduzi Cup visiwani Zanzibar jana, Januari 13.
Dkt. Kingwangalla amehoji kuwa hizo bilioni nne ambazo Mo amelipa kama mishahara ndani ya klabu hiyo zimefanyika kwa makubaliano gani na kwa kujiondoa kwake katika nafasi hiyo, mishahara itaendelea kulipwaje?.
aada ya mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup kumalizika kwa Simba kupoteza kwa bao moja mbele ya Mtibwa Sugar, bilionea Mo Dewji akaandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuwa hatoendelea na nafasi yake, atabakia kama mwekezaji na nguvu kubwa ataiwekeza kwenye miundombinu na soka la vijana.
It’s a pity simba couldn’t win. After paying salaries of close to 4 billion a year. I resign as the chair of the board and will remain as an investor. Simba Nguvu moja. I will focus on developing infrastructure and a youth academy!— Mohammed Dewji MO (@moodewji) January 13, 2020
0 Comments