BETI NASI UTAJIRIKE

WAWA,NYONI ,TSHABALALA NA KAPOMBE WAPEWA ONYO KALI

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wanahitaji kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza kwenye safu ya ulinzi ili kuhakikisha hawaruhusu mabao kizembe
Mbelgiji huyo ametoa kauli hiyo jana


baada ya mchezo wa raundi ya nne kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Mwadui Fc, mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

Katika michezo ya hivi karibuni safu ya ulinzi imekuwa ikiruhusu wastani wa bao moja kwenye kila mchezo.Waliruhusu mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Yanga, wakaruhusu mabao mawili kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na pia wameruhusu mabao matatu kwenye michezo mitatu iliyopita

"Tunaruhusu mabao mepesi, sio jambo jema. Tuna tatizo katika kujipanga na mawasiliano. Tutafanyia kazi changamoto hiyo ingawa hatuna muda wa kutosha kutokana na kuwa na mechi nyingi katika kipindi cha siku tisa zijazo," alisema Vandenbroeck

Akizungumzia mchezo huo, Vandenbroeck alisema timu yake iliicheza vizuri pamoja na kukabiliwa na changamoto za hapa na pale.Aidha Vandenbroeck ameongeza program za mazoezi kwa wachezaji wake baada ya kubaini kuna changamoto ya utimamu wa mwili kwa baadhi ya wachezaji

Jana baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao ulipigwa uwanja wa Taifa, wachezaji walibaki dimbani hapo kuendelea na mazoezi

Post a Comment

0 Comments