BETI NASI UTAJIRIKE

NINI KINAENDELEA KATI YA TFF NA SIMBA MPAKA MALALAMIKO YAENDE FIFA ?

Uongozi wa klabu ya Simba unafikiria kuandika barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuomba usaidizi ili kupata ITC za wachezaji wapya Shiza Kichuya na Luis Miquissone


Inaelezwa vyama vya soka vya Msumbiji na Misri vimeweka ngumu kutoa vibali vya nyota hao.Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema kumekuwa na ugumu kupata ITC za wachezaji hao lakini hawafahamu tatizo liko wapi hivyo kama italazimu wataomba usaidizi wa FIFA ikiwezekana wapewe vibali vya muda ili wachezaji waanze kucheza

"Luis na Kichuya wote wana tatizo moja ambalo ni kutopata ITC, kibali cha Luis kipo Msumbuji wakati Kichuya kipo Misri. Kuna mabishano kadhaa kwa pande za FA na klabu zao walizokuwa wakizichezea hivyo, tunataka kuiomba Fifa watupe vibali vya muda ili tuweze kuwatumia wachezaji hao wakati mengine yanaendelea.

"Hatufahamu tatizo hasa ni nini, kama ni ishu ya kimkataba ama la, ndiyo maana tunataka kwenda Fifa, ambapo pengine tutapata ufumbuzi na kujua tatizo. Kwa upande wetu tunafanyia kazi mchakato huu maana yote ni sahihi ingawa wachezaji wanachelewa kuanza kucheza,”  alisema Senzo 

Hata hivyo mapema jana Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu alisema ITC ya Kichuya tayari imewasili na anaweza kucheza mchezo dhidi ya Mwadui Fc hapo kesho kama kocha Sven Vandenbroeck atampa nafasi

Post a Comment

0 Comments