BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA WA SIMBA ACHANGANYWA NA KICHUYA ,MIQUISSONE NA KAHATA

Ukweli ni kwamba klabu ya Simba ndio timu iliyokamilika zaidi kwenye eneo la kiungo kuliko timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu mismu huu.Ikiwa imewaongeza Luis Miquissone na 


Shiza Kichuya kwenye usajili wa dirisha dogo, Simba sasa imesheheni mafundi kwelikweli jambo ambalo litawapa mtihani wakufunzi wa timu hiyo Sven Vandenbroeck na Selemani Matola.Hata kabla ya kuwaongeza Kichuya na Miquissone, vita ya kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza haikuwa nyepesi

Wachezaji Francis Kahata, Hassan Dilunga, Miraji Athumani, Ibrahim Ajib na Caltous Chama wamekuwa wakichuana vikali katika eneo la kiungo mshambuliajiujio wa Kichuya na Miquissone unakwenda kukoleza ushindani katika eneo hilo

Kichuya, Miquissone, Kahata kazi ipo
Nyota hawa huenda wakawa na ushindani wa kipekee kwani wana vitu vgingi vinavyofananawote wanatumia miguu ya kushoto, wabunifu na hodari wa kutengeneza nafasi huku Miquissone akiwa na takwimu nzuri zaidi katika kuzifumania nyavu

Kichuya anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao
Msimu wa 2017-18 alitengeneza mabao 26. Kahata msimu huu tayari amehusika kwenye mabao matatu ya Simba huku mwenyewe akifunga mawili
Kazi itabaki kwa benchi la ufundi kuwatumia ili wawe na manufaa kwa timu

Post a Comment

0 Comments