BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI: KWA SIMBA YA SVEN HAUMUHITAJI KAGERE WALA BOCCO KUPATA USHINDI

 Kocha Mkuu wa Simba, amejijengea ngome ya kufunga mabao kwa kutumia viungo msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara. Viungo wa timu hiyo tangu wacheze chini ya Sven ambaye alichukua mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa,

 wamefunga mabao 16 katika michezo sita aliyosimamia kocha huyo.Mabao hayo ni tofauti ya matatu dhidi ya yale yaliyofungwa wakati timu ikifundishwa na Aussems ambaye kabla ya kuondolewa, aliiongoza Simba kwenye mechi 10 za Ligi Kuu Bara msimu huu.

Aussems alikuwa akitumia zaidi  washambuliaji na kwenye mabao  19, washambuliaji walifunga 14 na viungo mabao matatu,mabeki mawili.

Miraji Athuman alifunga sita na Meddie Kagere (8), hao ndiyo washambuliaji. Upande wa viungo, Clatous Chama, Francis Kahata na Deo Kanda, kila mmoja alifunga bao moja kama ilivyo kwa mabeki Tairone Santos na Mohamed Hussein.

Sven, akiwa ameiongoza timu yake kufunga mabao 16 kwenye mechi sita, viungo wamefunga jumla ya mabao 13 na mshambuliaji mmoja pekee amefunga mabao matatu.
Kagere mabao matatu, Dilunga (4), Deo Kanda (3), Kahata na Jonas Mkude kila mmoja amefunga mawili, huku Gerson Fraga na Chama wakifunga mojamoja.

Simba ya Sven huenda ikavunja rekodi ya mabao 19 ya Aussems kwenye mechi 10 za mwanzo kwani amebakiwa na mechi nne mkononi kufikia idadi hiyo ya mechi 10

Post a Comment

0 Comments