Jambo ambalo limewafanya baadhi ya wachezaji nyota wa Afrika Barani Ulaya kupata wakati mgumu kuchagua baina ya klabu zao na mataifa yao.
Mjadala ambao wengi waliamini hatimaye umefikia tamati mwaka 2019.lakini mwaka 2021 mjadala huo utarejea tena kwenye duru za kandanda baina ya Afika na Ulaya.Si jambo jengine bali ratiba ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mwaka 2019 mashindano hayo yalifanyika mwezi Juni kama ambavyo wachambuzi wengi ndani na nje ya bara walivyokuwa wakishauri kwa muda mrefu.Lakini kwa mwaka 2021 tarehe ya mashindano imerejeshwa mwezi wa Januari kama ilivyokuwa zamani.
Mwezi Januari ni kipindi ambacho ligi za Ulaya zinakuwa katikati na ushindani unakuwa mkubwa, hivyo makocha wengi hawafurahii kuwaachia wachezaji wao nyota kurejea Afrika.
Baadhi ya wachezaji wamewahi kususia moja kwa moja ama kutafuta sababu ili wasirejee kwenye mataifa yao mwezi Januari kulinda vibarua vyao kwenye klabu.
Wachezaji hao nyota wa Afrika hukaa mpaka wiki tano na timu zao za taifa na hukosa mpaka michezo mitano ya ligi na klabu zao.Mwezi Juni nikipindi kinachopendwa kwa kuwa ligi nyingi za Ulaya huwa kwenye mapumziko.
"Kwa kweli ratiba hiyo (ya mwezi Januari) inakuathiri mno unapofikiria kuwasajili wachezaji kutoka Afrika," kocha wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp ameiambia BBC.
"Na kwa hakika (wakirudi) baada ya michuano wanakuwa si kama walivyoondoka. Huwa hawarudi katika kiwango chao baada ya mashindano," amesisitiza.
"Unaposajili wachezaji, unalifikiria hilo na itakuwaje akienda kwenye mashindano ya Afrika, wakati mwengine unaamua: 'wacha nimuache mchezaji huyu'."
Vinara wa Ligi ya EPL Liverpoolmathalani wanaweza kuwakosa nyota wao tegemezi watatu kutokana na mabadiliko hayo mwakani ambao ni Sadio Mane, Mohamed Salah na Naby Keita kwa mwezi mmoja.
Kwa nini mashindano yamerudi January?
Shirikisho la Kandanda Africa (CAF) lieeleza kuwa mashindano yajayo yatafanyika nchini Cameroon kati ya Januari 9 mpaka Februari 6.
Kwa mujibu wa CAF uamuzi huo umefikiwa baada ya kupata ripoti kutoka Cameroon zinazoeleza kuwa kipindi cha Juni kitakuwa kigumu kwa hali ya hewa.
Mabadiliko hayo pia yanamaanisha kuwa mashindano ya Afrika hayataangukia katika wakati sawa na mashindano ya kombe la dunia la vilabu litakalofanyika Uchina Juni 2021.
Wachezaji wa EPL ambao wanaweza kukosekana Januari 2021?
Endapo mataifa yao yote yatafuzu, hawa ndio wachezaji wa Afrika ambao kwa sasa wanachezea katika vilabu vya Ligi ya Primia ambao wanaweza kuondoka na kwenda kuwakilisha mataifa yao:
Arsenal - Pierre-Emerick Aubmaeyang (Gabon), Nicolas Pepe (Ivory Coast), Mohamed Elneny (Misri - kwa sasa yupo kwa mkopo Besiktas)
Aston Villa - Marvelous Nakamba (Zimbabwe), Trezeguet (Misri), Jonathan Kodjia (Ivory Coast), Ahmed Elmohamady (Egypt)
Brighton - Leon Balogun (Nigeria), Yves Bissouma (Mali), Gaetan Bong (Cameroon), Percy Tau (Afrika Kusini - kwa sasa yupo kwa mkopoBrugge)
Crystal Palace - Jeffrey Schlupp (Ghana), Cheikhou Kouyate (Senegal), Jordan Ayew (Ghana), Wilfried Zaha (Ivory Coast)
Everton - Alex Iwobi (Nigeria), Jean-Philippe Gbamin (Ivory Coast), Oumar Niasse (Senegal), Yannick Bolasie (DR Congo - kwa sasa yupo kwa mkopo Sporting Lisbon)
Leicester City - Kelechi Ịheanachọ (Nigeria), Wilfred Ndidi (Nigeria), Daniel Amartey (Ghana), Islam Slimani (Algeria - ckwa sasa yupo kwa mkopo Monaco), Rachid Ghezzal (Algeria - kwa sasa yupo kwa mkopo Fiorentina)
Liverpool - Naby Keita (Guinea), Mohamed Salah (Misri), Sadio Mane (Senegal). Joel Matip (Cameroon) amestaafu soka la kimataifa.
Manchester City - Riyad Mahrez (Algeria)
Manchester United - Eric Bailly (Ivory Coast)
Newcastle - Christian Atsu (Ghana), Henri Saivet (Senegal)
Southampton - Moussa Djenepo (Mali), Sofiane Boufal (Morocco), Mario Lemina (Gabon - kwa sasa yupo kwa mkopo Galatasaray)
Tottenham - Victor Wanyama (Kenya), Serge Aurier (Ivory Coast)
Watford - Isaac Success (Nigeria), Ismaila Sarr (Senegal)
West Ham - Arthur Masuaku (DR Congo)
Wolves - Romain Saiss (Morocco)
SOURCE : BBC
0 Comments