BETI NASI UTAJIRIKE

TIMU YA SAMATTA YAANZA KUTOA VIPIGO UINGEREZA

Mshambuliaji wa kimataif Mbwana Ally Samatta anayekipiga klabu ya Aston Villa amefika na bahati baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa Villa ParkWatford walikuwa wakwanza kupata bao kupitia kupitia Troy Deeney dakika ya 38 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa  hilo  1. Kipindi cha pili kilianza na Douglas Luiz alichomoa bao hilo dakika ya 68 huku Tryone Mings akishindilia bao la pili dakika ya 90+5 na kuifanya Aston Villa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Kwa matokeo hayo Aston Villa imepanda mpaka nafasi ya 16 kutoka 18 waliyokuwa kabla ya kuwasili Mbwana Samatta. Klabu hiyo imecheza jumla ya michezo 24 ikishinda michezo 7 sare 4 na kufungwa 13 ikiwa na pointi 25 .

Ujio wa Mbwana Samatta 

Tangu kuanza kwa mwaka 2020 klabu hiyo imecheza jumla ya michezo 6 huku ikishinda michezo miwili tu dhidi ya Burnley na Watford. Mara ya mwisho kupata ushindi kabla ya kuwasili Samatta ni tarehe 01-01-2020 dhidi ya Burnley. Usajili wa Mbwana Samatta umeamsha ari ya mashindano kwa timu hiyo na sasa watapambana wasiweze kushuka daraja.

Mshambuliaji Mbwana Samatta amekwishaanza mazoezi rasmi na klabu hiyo na tunaweza kumuona kwenye mchezo dhidi ya Leicester City utakaopigwa tarehe 28 mwezi januari kwenye dimba la Villa Park. 

Post a Comment

0 Comments