BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU TAREHE 27-01-2020

Tottenham wanasuka mipango ya kumrejesha mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi. (Express)
Manchester United wanaweza kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo yao hayataboreka msimu huu, huku kocha timu ya taifa ya England Gareth Southgate akipigiwa upatu kumrithi Solskjaer. (Mail)
Barcelona hawatarajiwi kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, na badala yake wanaelekeza nguvu zao kwa mshambuliaji wa Valencia Rodrigo Moreno, 28. (Sport)

Arsenal striker Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya picha

Aubameyang hata hivyo anaweza kusajiliwa na Paris St-Germain kama mbadala wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32. (Foot Mercato - in French)
Cavani, anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu kadhaa zikiwemo Chelsea na Manchester United. Mchezaji huyo amekubali, japo kwa mdomo tu, kuhamia klabu ya Atletico Madrid kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi. (Goal.com)
Cavani amekataa mapendekezo ya mkataba wa mshahara wa Pauni milioni 10 kwa mwaka na marupurupu tele uliowasilishwa na Manchester United. (Mirror)
Tottenham na Aston Villa wamegonga mwamba kumsajili mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic baada ya timu hizo kushindwa kutoa dau la Pauni milioni 40 kwa klabu ya Fulham.

Mohamed Salah and Pablo MariHaki miliki ya picha

Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Flamengo ya Brazil Pablo Mari, 26. (Mail)
Mitrovic, 25, anaweza kuchagua kuikacha Fulham mwishoni kwa msimu endapo klabu hiyo itashindwa kupanda daraja na kurudi katika Ligi ya Primia. (Star)
Manchester United bado wanavutiwa na kiungo wa Sporting Lisbon Mreno Bruno Fernandes, 25, lakini klabu hizo mbili bado hazijaafikiana juu ya bei ya usajili wa kiungo huyo. (A Bola - in Portuguese)

Marocs Rojo in action during a pre-season friendly against LeedsHaki miliki ya picha

Marcos Rojo, 29, anarejea kwa mkopo katika klabu Estudiantes - baada ya Manchester United kushindwa kupata klabu inayotaka kumnunua beki huyo wa Argentina. (Mirror)
Southampton wamefanya mazungumzo zaidi na Tottenham juu ya usajili wa beki wa pembeni Kyle Walker-Peters, 22. (Mail)
Birmingham City wanatarajiwa kukataa ofa za usajili wa mchezaji wao kinda Jude Bellingham, 16, wakiamini kuwa wanaweza kuendelea kubaki naye licha ya kunyemelewa na vigogo Manchester United na Liverpool. (90 Min)

Post a Comment

0 Comments