BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI TAREHE 05-01-2020

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Ujerumani Toni Kroos, 29, huenda akahamia Manchester United kama sehemu ya mkataba wa kumpeleka Paul Pogba, 26, katika klabu hiyo ya Uhispania. (Sun)
Juventus inapani akumpatia kiungo wa Ufaransa Adrien Rabiot, 24, katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji na pesa kwa mchezaji wao wa zamani,Pogba. (Sun)
Arsenal pia wanataka kumsajili beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng, 31. (Sky Sports)

Jerome BoatengHaki miliki ya picha

Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro chausajili wa beki wa Norwich Max Aarons lakini Tottenham huenda ikapata nafasi ya kumsajili kiungo huyo wa miaka 19. (Daily Mail)
Gunners imeelekeza darubini yake kwa Boateng licha ya tetesi kuwa huenda wa RB Leipzig ikilipa pesa nyingi kumpata bekiwa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (Evening Standard)
Manchester United imejaribu kupita ajenti Mino Raiola wakati walipotaka kumsaini mshambuliaji wa Norway Erling Haaland kutoka Red Bull Salzburg. Kiungo huyo wa miaka 19- hata hivyo aliamua kujiunga na Borussia Dortmund. (Daily Mail)

Erling HaalandHaki miliki ya picha

Kiungo wakati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, anakaribia kujiunga na Inter Milan. (Ekstra Bladet, in Danish)
Borussia Dortmund haina mpango wa kumuuza winga wa England Jadon Sancho, 19, kwa Chelsea hadi angalau mwisho wa msimu huu na The Blues pia watalazimika kusubiri kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Goal.com)
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone amepuuzilia mbali tetesi za kiungo wa kati wa Ufaransa Thomas Lemar wa miaka 24 - mbaye amehusishwa na Tottenham na Arsenal - anaondoka klabu hiyo. (Mirror)

Jadon SanchoHaki miliki ya picha

Chelsea, Crystal Palace na Brighton ni miongoni mwa klabu zinamng'ang'ania mshambuliaji wa CSKA Moscow Mrusi Fedor Chalov, 21. (Sky Sports)
Aston Villa huenda ikamnunua kipa wa zamani wa Burnley Joe Hart, 32, baada ya kumkosa mchezaji mwenzake wa zamani Clarets Tom Heaton kutokana na jeraha la muda. (Daily Mail)
Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27, pamoja na mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 24, waliondolea kwenye mazoezi na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kuwa wagonjwa dakika 15 baada ya kufika uwanjani. (ESPN)

Jesse LingardHaki miliki ya pichan

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amedokeza kuwa alihojiwa kuhusu kazi ya Liverpool baada ya Brendan Rodgers kufutwa kazi Oktoba 2015,lakini akishindwa na Jurgen Klopp. (Telegraph)
Bilionea na mwenye hisa wa Arsenal, Alisher Usmanov anatafakari wazo la kuungana na mshirika wake wa kibiashara na mmilikik wa Everton Farhad Moshiri kwa kuwekeza katika klabu ya Merseyside. (Times, subscription required)

Post a Comment

0 Comments