BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA TAREHE 03/01/2019

Manchester United inajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kwa Real Madrid au Juventus mwezi huu, lakini wanataka £150m. (Express)
Manchester United inapania kuwanunua viungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na James Maddison, 23, kutoka Leicester. (Independent)
Wachezaji wengine wanolengwa na United ni kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can, 25, na Sean Longstaff, 22, wa Newcastle. (ESPN)

James MaddisonHaki miliki ya picha

Aston Villa ina mpango wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudmu. (Footmercato - in French)
Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. 
Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ameelezea kujitolea kwake kwa Arsenal na kutuliza tetesi za kuondoka kwake mwezi Januari. (Evening Standard)

Gabon Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya picha

Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Telegraph)
Inter Milan ni moja ya klabu zilizowasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen. Kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 27 inakamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Manchester City inatarajiwa kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34. (Sun)

FernandinhoHaki miliki ya picha

Dau la Chelsea la yuro milioni 40 la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele ,23, limekataliwa na Lyon. (Footmercato - Kwa Kifaransa)
Aston Villa inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua kipa wa Stoke City Muingereza, Jack Butland, 26. (Mail)
Ajax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen kwa sababu bei ya mchezaji huyo wa miaka 32 ni ghali sana . (De Telegraaf - Ujerumani)

Jan VertonghenHaki miliki ya picha

Southampton wanataka kumsaini beki wa Valladolid raia wa Ghana Mohammed Salisu, 20. (Sky Sports)
Leicester imeipiku Arsenal katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Juventus na Italia, Daniele Rugani, 25. (Express)
Arsenal imemuulizia winga wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Marca - ya Uhispania)

Thomas LemarHaki miliki ya picha

Post a Comment

0 Comments