BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 20-01-2020

Bruno Fernandes, 25, ameambia Sporting Lisbon anataka kujiunga na Man United na mazungumzo zaidi yamepangwa wiki hii baada ya kugonga mwamba kuhusu thamani ya mchezaji huyo wa Portugal. (Sky Sports)
Beki wa Paris St-Germain na Ufaransa Layvin Kurzawa, 27, atajiunga na Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwezi Juni na amekubali mkataba wa miaka mitano na The Gunners.. (France Football - in French)
Arsenal itajaribu kumsaini beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng, 31, kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuwasilisha ombi la £50m ili kumnunua beki wa kati wa Ufaransa na klabu ya RB Leipzig Dayot Upamecano, 21, mwisho wa msimu. (Star)
Jerome Boateng
Inter Milan inataka kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, kwa wakati mzuri ili aweze kushiriki katika mechi ya ligi ya Serie A dhidi ya klabu ya Cagliari mnamo tarehe 26 mwezi Januari. (Mail)
Afisa mkuu wa klabu ya Inter Beppe Marotta anasema kwamba klabu hiyo ina hamu ya kumsaini winga wa Chelsea Victor Moses, 29, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce, pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo Olivier Giroud, 33, mbali na Eriksen. (Sky Sports)
Antonio Conte amemshutumu Jose Mourinho kwa kubadilisha maneno yake baada ya mkufunzi huyo wa Spurs kumkosoa mwenzake wa Inter kwa kuzungumzia kuhusu mchezaji wake Eriksen. (Mirror)
Jose MourinhoHaki miliki ya pichao
Inter Milan pia ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Croatia Luca Modric , 34, kutoka Real Madrid(Sport - in Spanish)
Atletico Madrid imeipatia Paris St-Germain Yuro milioni 10 (£8.5m) ili kumnunua mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32. (L'Equipe - in French)
Tottenham huenda ikamnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 31, ambaye kwa sasa anacheza Monaco kwa mkopo. (Telegraph)
Islam SlimaniHaki miliki ya picha
Leicester na Aston Villa zinamlenga mshambuliaji wa Ufaransa Serhou Guirassy, 23, kutoka klabu ya Ligue 1 Amiens mwezi Januari. (Mail)
Maombi ya Manchester City na Barcelona ya kutaka kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Alessandro Bastoni, 20, yamekataliwa. (La Gazetta dello Sport - in Italian)
Liverpool inafikiria kumsajili kinda wa Portugal na klabu ya Nice mwenye umri wa miaka 17 Pedro Brazao. (RMC Sport, via Mail)
Klabu ya Lyon ina hamu ya kumsajili beki wa Athletico Bruno Guimaraes, 22, ambaye pia ameripotiwa kunyatiwa na Arsenal. (L'Equipe - in French)
Real Madrid itatangaza usajili wa dau la 30m euro (£25.6m) la mchezaji wa Flamengo's Reinier Jesus siku ya Jumatatu wakati ambapo kiungo huyo wa kati wa Brazil amefikisha miaka 18. (AS)

Post a Comment

0 Comments