BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 06-01-2020

Manchester United wamefufua tena juhudi za kumsajili nyota wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25. (Goal.com)
Barcelona iko mbioni kumsaka Dani Olmo wa Dinamo Zagreb licha ya nyota huyo kung'ang'aniwa na Chelsea na Manchester United ambapo tayari wamefanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo wa Uhispania wa miaka 21. (Goal.com)
Arsenal wamewasilisha ombi rasmi kwa Bayern Munich kuhusu usajili wa beki wa wa Ujerumani Jerome Boateng, 31. (Footmercato - in French)
Jerome Boateng, Mats Hummels na Thomas MullerHaki miliki ya pichaAFP
Image captionJerome Boateng, Mats Hummels na Thomas Muller
Mchezaji wa safu ya kati ya Ajax Mmorocco Hakim Ziyech, 26, ameambiwa kuwa anaweza kuondoka klabu hiyo mwezi huu, baada ya kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Arsenal na Tottenham mwezi huu wa Januari. (Football.London)
Chelsea imeanza mkakati wa kumsaka mshambuliaji wa Inter Milan na Brazil Gabriel Barbosa, 23, mwezi huuwa Januari Frank Lampard akipania kumsajili mshambuliaji mpya. (Daily Express)
Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27, ameungana na ajenti Mino Raiola, baada ya tetesi kuzuka kwamba huenda akaondoka Old Trafford. (Mail)
Jesse LingardHaki miliki ya picha
Lampard amempatia ishara mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kuondoka Chelsea mwezi huu licha ya tetesi zinazomhusisha na Aston Villa. (Birmingham Mail)
Watford imeungana na Everton katika kinyang'anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Carlisle wa miaka 17- Muingereza Jarrad Branthwaite. (Watford Observer)
Mashabiki wa Liverpool wamevutiwa na mpango wa usajili wa Ousmane Dembele, baada ya mshambuliaji huyo wa miaka 22- wa Barcelona na Ufaransa kubonyeza Like, picha inayomonesha akiwa amevalia jezi nyekundu nstagram . (Daily Express)
Winga wa Barcelona Ousmane DembeleHaki miliki ya picha
Mkufunzi wa Sheffield United Chris Wilder anapania kumnunua mshambuliaji wa CFR Cluj Mfaransa Billel Omrani, 26, mwezi huu. (Sun)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anawasaka wambuliaji wawili mwezi huu wa Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (South London Press)
Beki wa Burnley Ben Gibson, 26, ananyatiwa na klabu ya Eintracht Frankfurt na Cologne nchini Ujerumani. (Daily Mail)
Roy HodgsonHaki miliki ya picha
Man United wako tayari kutoa kiasi cha Pauni million 45 ili kumnasa nyota wa Leicester City James Maddson na watamtoa Jesse Lingard ili kuweza kufanikisha usajili huo.
West ham watapigana vikumbo na Man City katika kuwania saini ya beki kisiki wa Napoli Kalidou Koulibali. (Sunday Express)
Kalidou KoulibalyHaki miliki ya picha
Inter Milan wanataka kumsajili kiungo wa Spurs Christian Eriksen kwa dau la pauni million 20 katika dirisha hili la januari licha ya nyota huyo atakuwa huru kuondoka bure mwishoni mwa msimu. (Sun on Sunday)
Juventus wamefanya mazungumzo ya awali na Chelsea ili kuangalia uwezokano wa kumsajili beki wa kushoto wa timu hiyo mbrazil Emerson.

Post a Comment

0 Comments