BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATAO TAREHE 08-01-2020

Chelsea wanavutiwa kumsajili winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha mwezi huu lakini hawako tayari kufikia dau la pauni milioni 80 lililotajwa na klabu hiyo. (Express)


Manchester City wanawania kumsajili winga wa Wolves Mhispania Adama Traore, 23. (Calcio Mercato, via Manchester Evening News)
Wakala wa kiungo wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 32, atafanya mazungumza na Manchester United kuhusiana na uwezekano wa mchezaji huo kuhamia United mwezi huu. (Corriere Della Sera, via Mirror)
Aston Villa wako kwenye mawasiliano na Crystal Palace kuhusu kumrejesha mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 29. (Telegraph, via Birmingham Mail)
Villa wamepewa fursa ya kumsajili kipa mkongwe Pepe Reina, 37, kutoka AC Milan. (Mail)

nahodha wa Manchester United Ashley Young, 34

Inter Milan inaripotiwa kumfuatilia nahodha wa Manchester United Ashley Young, 34. (Manchester Evening News)
Mario Gotze, ambaye alifunga goli la ushindi la Ujerumani katika fainali la kombe la dunia 2014 anajiandaa kuondoka katika klabu ya Borussia Dortmund kwa uhamisho huru pale mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Bild, via Mirror)
Newcastle wanavutiwa kumsajili winga wa zamani wa Liverpool, Ryan Babel kutoka Galatasaray. Klabu hiyo ya Uturuki imepanga kumuachia Mholanzi huyo mwezi huu huku klabu ya Ajax ipia ikimpigia hesabu. (Express)

Kocha Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya picha

Kocha Ole Gunnar Solskjaer amesema wachezaji wengi wa Man United wanacheza kwa ajili ya kesho yao. Kiungo wa England Jesse Lingard, 27 amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake pamoja na kiungo Mserbia Nemanja Matic. Beki wa Mholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22 na beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 25 watamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)
Everton inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Juventus mfaransa Adrien Rabiot, 24 mpaka mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)
Mshambuliaji wa Ujerumani Leroy Sane, 23, anakaribia kurejea kwenye mazoezi ya Manchester City baada ya kuwa nje kwa miezi mitano akiunguza majeraha. (Manchester Evening News)
Napoli wanavutiwa na mshambuliaji wa Brighton mfaransa Neal Maupay 23. (Telegraph)

Post a Comment

0 Comments