BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 22-01-2020


Inter Miami imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 31, na David Silva, 34, ambao wataondoka klabu hiyo msimu wa joto. (Sun)
Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kwa mkataba wa £55m mwisho wa wiki hii baada ya kuafikiana na Sporting Lisbon. (Mirror)
Fernandes aliwapuuza mashabiki wa Sporting na kusukuma kamera za televisheni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Braga siku ya Jumanne katika kile kilionekana kuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo. (Star)
Bruno FernandesHaki miliki ya picha
Manchester United imetoa ofa ya zaidi ya £30mkumnunua kiungo wa kati wa Birmingham City wa miaka 16 Jude Bellingham. (Sun)
Mkufunzi wa Barcelona Quique Setien anasema kuwa klabu hiyo inamtafuta mchezaji atakayeziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wa Uruguay aliyeumia Luis Suarez, 32 mwezi huu. (Sport)
Barca inapania kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Rodrigo Moreno lakini Valencia inataka kumnunua kiungo huyo kwa euro milioni 60. (Marca)
Rodrigo MorenoHaki miliki ya picha
Liverpool wako tayari kumuuza Xherdan Shaqiri kwa £25m msimu wa joto lakini haitaki kumuachilia winga huyo wa Uswizi wa miaka 28, aondoke kwa mkopo mwezi huu. (Liverpool Echo)
Beki wa Real Madrid, Mhispania Alvaro Odriozola, 24, ametua Ujerumani kukamilisha uhamisho wake kwenda Bayern Munich hadi msimu utakapokamilika. (AS - in Spanish)
Barcelona inamtaka Pierre-Emerick Aubameyang lakini kuondoka kwake Arsenal kabla ya mkataba wake kuisha mwaka 2021 huenda kukamgharimu mshambuliaji huyo wa Gabon, 30, £15.15m. (Star)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya picha
Bournemouth wanamtaka kumnunua mshambuliaji wa Lyon -anayekadiriwa kuwa na thamani ya £35 Bertrand Traore. (Mail)
Leicester na West Ham pia wanamfuatilia Traore, 24, ambaye ni mchezaji huyo kimataifa wa Burkina Faso. (Foot Mercato - in French)
Burnley, Leicester na Sheffield United wanamtaka kiungo wa kati wa Bristol City Josh Brownhill, 24. (Bristol Post

Post a Comment

0 Comments