BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 15-01-2020

Paris St-Germain ipo tiyari kupambana na Inter Milan kumuwania kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Mirror)


Mkurugenzi mtendaji wa Atletico Madrid Maguel Angel Gil Marin, alikuwa jijini Paris kufanya mazungumzo na PSG kuhusu mshambuliaji wao Edinson Cavani, 32. (Marca)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexanndre Lacazette, 28, ni pendekezo la Atletico Madrid iwapo hawatampata Cavani. (Sky Sports)
Manchester City imeondoa uwezewekano wa mlinzi wake wa kati Muingereza John Stones, 25, kujiunga na miamba ya London Arsenal katika dirisha hili la usajili. (Manchester Evening News)
Kocha Pep Guardiola hana nia ya kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (Telegraph)
Cavani alijiunga na PSG mwaka 2013Haki miliki ya pichan
Chelsea haina uhakika wa kutoa paundi milioni 40 kumnunua mlinzi wake wa zamani Muholanzi Nathan Ake,24 na pia hawatamsajili mchezaji mwenzake wa Bournemouth raia wa Uingereza Callum Wilson, 27. (Sky Sports)
Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward ameonekana akisafiri kuelekea Ufaransa kwa kutumia treni ya Eurostar, United inapania kumsajili kiungo wa Lile mfaransa Boubakary Soumare, 20. (Star)
United itatakiwa kulipa pauni milioni tano kumfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer. (Sun)
Wakala wa winga wa United Mholanzi Tahith Chong, 20, ameonekana Inter Milan huku mchezaji huyo akitarajia kuondoka Old Trafford. (Mirror)
Guardiola anatajwa kuwa miongoni mwa makocha bora zaidi kuwahi kutokea
Mlinzi wa Ranger raia wa Ireland ya Kaskazini Danny Finlayson, 18, na mlinzi wa kushoto wa Uskochi Matthew Shiels, 19, wanatarajiwa kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Marekani ya Orange County. (Daily Record)
Mashambuliaji wa Los Angeles FC Carlos Vela atamkaribisha mshambuliaji wa Sevilla Javier Hernandez , hata kama mchezaji huyo mwenye miaka 31 atacheza na wapinzani wao LA Galaxy. (ESPN)
Mlinda mlango raia wa Ufilipino Neil Etheridge, 29, hatokuwemo katika kikosi cha Cardiff City kitakachoumana na Carlisle katika mzunguko wa tatu wa kombe la FA huku tetesi za yeye kuhamia Westham zikiendelea kushika kasi.(Wales Online)
Inter Milan inamuwinda mlinzi wa Parma Matteo Darmian, 30 .(Tuttomercatoweb - in Italian)
Mshambuliaji wa zamani Darren Bent ametaka kujumuishwa kwa mlinzi wa kushoto wa Manchester United Brandon Williams, 19 katika michuano Euro 2020. (Talksport)

Post a Comment

0 Comments