BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 21-01-2020

Manchester United inaandaa ofa ya £43m kumnunua mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, baada ya Marcus Rashford kuumia mgongo. (Foot Mercato, via Manchester Evening News)
Manchester United watalazimika kulipa ada ya juu ya uhamisho kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, mwezi huu badala ya kumchukua kwa mkopo - lakini mchezaji huyo yuko tayari kuondoka PSG. (Manchester Evening News)
Edinson CavaniHaki miliki ya picha
Kujiunga na Liverpool ndio "lengo kuu" la mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23, ambaye anataka kucheza katika ligi kuu ya premia. (Bild, via Sport Witness)
Inter Milan wanakaribia kumsajili kwa mkopo beki wa Chelsea Victor Moses, 29, kujiunga na mkufunzi wake wa zamani Antonio Conte. Fenerbahce, klabu ambayo kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria anachezea kwa mkopo imeridhia kumuachilia. (Mail)
Mkufunzi wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anasema Gunners "ilituvunja moyo" lipoondoka Highbury na kuhamia uwanja wa Emirates. (Evening Standard)
Victor MosesHaki miliki ya picha
Everton imekataa ofa mbili za kumnunua beki Mason Holgate, huku Newcastle, Bournemouth na Sheffield United zikiwa miongoni mwa timu zinazomtaka mchezaji huyo wa miaka 23. (Football Insider)
Liverpool haiko tayari kumpoteza kiungo wa kati wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, licha ya Roma kuonesha nia ya kutaka kumnunua mwezi huu. (Sky Sports)
Manchester United imekiri kuwa ilishindwa na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha usajili wa kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 22. (Star)
Manchester United imekiri kuwa ilishindwa na Real MadridHaki miliki ya picha
Klabu ya Uhispania ya Celta Vigo imekuwa ikiwasiliana na Southampton kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati, Oriol Romeu lakini Saints hawataki Mhispania huyo wa miaka 28-kuondoka (Southern Daily Echo)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie ameionya United kutokimbilia kumrudisha uwanjani Marcus Rashford, 22, baaada ya kiungo huyo mshambulizi kuumia mgongo. (Manchester Evening News)
Bournemouth wanamtaka winga wa Borussia Dortmund Jacob Bruun Larsen, 21, lakini mkufunzi wa Cherries Eddie Howe amesema hakuna mchezaji mpya atakayejiunga nao. (Daily Echo)

Post a Comment

0 Comments