BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 14-01-2020

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anahofu kuwa mshambuliaji wa kikosi hicho Harry Kane, 26 atakuwa nje ya uwanja mpaka msimu ujao na atakosa michuano ya Euro 2020 kutokana na jeraha. (Sun)

Mourinho anahitaji washambuliaji wawili Januari hii kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kane. Mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piatek, 24, ni mmoja kati ya wachezaji wanaotupiwa macho sambamba na mshambuliaji wa Napoli Fernando Llorente 34 na mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke, 29. (Independent)
Mshambuliaji Thomas Mular ataondoka Bayern Munich baada ya miaka 20 kuwa na klabu hiyo. (Sport 1, via Sun)
PiatekHaki miliki ya picha
Kiungo wa timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, yuko karibuni kuiacha Tottenham baada ya kufikia makubaliano na Inter Milan ambapo atakuwa akilipwa pauni 100,000 kwa wiki.(Times)
Atletico Madrid imeamua mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 28 kuwa kipaumbele chao ikiwa watashindwa kumsajili Edinson Cavani, 32, mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Uruguay.(Express)
Mshambuliaji wa Southampton Danny Ings,27, anastahili nafasi kwenye kikosi cha Gareth Southgate, amesema kocha wa Leicester Brendan Rodgers, ambaye alimsajili kujiunga na Liverpool.(Sky Sports)
Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameshinda kesi dhidi ya klabu hiyo, ingawa amelipwa zaidi ya pauni 85,000 kama fidia.(Mirror)
Kocha wa Newcastle Steve Bruce atajadiliana na mmiliki Steve Bruce wiki hii kuhusu usajili wa mwezi Januari (Guardian)
Haki miliki ya picha
Liverpool imetoa ofa ya pauni milioni 12.8 kwa Trabzonspor kwa ajili ya kumnasa mlinda mlango Ugurcan Cakir,23. (Sabah, via Sport Witness)
Southampton imeendelea kushikilia msimamo wa kuwa kiungo wao Che Adams,23 hataondoka kwa mkopo mwezi Januari kwenda Leeds. (Mirror)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Alvaro Morata,27, alitapika kabla ya kipindi cha matuta katika mchezo wa fainali dhidi ya Real Madrid. (Marca)
Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, 62, amesema ana nia ya kuinunua Arsenal mwaka 2021.(Evening Standard)
Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn Martin Olsson,31, anatarajia kuwa mazoezini wiki nzima akiwa na West Brom. (Lancashire Telegraph)

Post a Comment

0 Comments