BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 25-01-2020

Barcelona wanataka kuushangaza ulimwengu kwa kumsaini mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud, 33. (Independent, via Mail)
Roma wana nia ya kumsaini mshambuliaji kutoka pembeni wa zamani wa Manchester United Adnan Januzaj, mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24.(Calciomercato)
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark atasaini mkataba utakaomuwezesha kulipwa pauni 320,000 kwa wiki.(Sky Sports)
Christian Eriksen
Kirungo wa Kati wa Tottenham  Christian Eriksen, 27, atasafiri hadi Milan am Ali atafanyiwa vipimo vya afya mapema wiki ijayo kabla ya kuhamia Inter. (Guardian)
Mashabiki wa Manchester United  wanapanga kujitokeza kwa wingi wakati wa mechi ya Primia Ligi dhidi ya Wolves katika Old Trafford tarehe 1 Februari. (Mirror)
Meneja wa Real Sociedad boss Imanwaol Alguacil anasema ataamua ikiwa Willian Jose anayelengwa na Tottenham atacheza dhidi ya Mallorca Jumamosi.
Gabriel Martinelli
Arsenal wanataka kumuongezea mshahara Gabriel Martinelli 18 kwa Pauni 30,000 kwa wiki ili kuepusha dhamira ya Real Madrid kutaka kumsaini mshambuliaji huyu kutoka Brazil. (Mail)
Manchester United pia wanataka kumuongezea mshahara kijana wao wa kimataifa wa England Angel Gomes, 19, ambaye mkataba wake unafika tamati msimu wa joto na ameunganishwa kutaka kujiunga na Chelsea. (Sun)
Christian BentekeHaki miliki ya picha
Aston Villa bado wanaonesha wanamuhitaji mchezaji wao wa zamani Christian Benteke, 29, ambae kwasasa ni mshambuliaji wa Crystal Palace na Ubelgiji.(Sport Witness)
Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Shanghai Shenhua's Odion Ighalo, 30, au Islam Slimani wa Leicester, 31, ambaye yupo kwa mkopo huko Monaco, kipindi hiki ambacho wanatafuta mbadala la Marcus Rashford ambaye ni majeruhi. (Sky Sports)
West Ham wamefungua mazungumzo na Amiens juu ya mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa wa miaka 25 Serhou Guirassy.(Football.London)
Liverpool inataka kuwapiku Real Madrid na Barcelona kumsaini kiungo wa Benfica U19 Rafael Brito, 18, ambaye mkataba wake una kifungu cha kutolewa cha pauni 38m.
Kocha mkuu wa Lille Christophe Galtier anakiri kuwa hana uhakika kama beki wa Ufaransa Boubakary Soumare, 20, aliyehusishwa na Manchester United, bado atakuwa klabuni hapo mwishoni mwa dirisha la uhamisho.(Goal.com)
Arsenal wanaripotiwa wapo katika mazungumzo na Atletico Madrid juu ya mpango wa kiungo wa Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Independent, via Mail)
mshambuliaji wa AC Milan, Krzysztof PiatekHaki miliki ya picha
Tottenham bado hawajajua hatma ya mshambuliaji wa AC Milan, Krzysztof Piatek yawezekana wakapambana hadi siku ya tarehe ya mwisho na Klabu ya Italia inataka pauni 30m kwa mchezaji wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 24. (Record via Star)
Tottenham inaweza kulazimishwa kupunguza hesabu yao ya £ 7m ya Victor Wanyama kwani bado wanapambana kupata mnunuzi wa kiungo wa Kenya mwenye umri wa miaka 28.
West Ham wametoa zabuni yenye thamani ya pauni 12m kwa Nottingham Forest ili kumsaini beki wa kulia Matty Cash mwenye umri wa miaka 22.(Sky Sports
West Ham wanapo mbioni kutengeneza zabuni ya euro 25m (£ 21m) kusaini kiungo wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 24, kutoka Slavia Prague.

Post a Comment

0 Comments